Saturday, October 7, 2017

JE,KUNA TATIZO KUBWA LA MATUMIZI YA UMEME NYUMBANI KWAKO AU OFFISINI KWAKO?



>>Swali kutoka kwa mteja wetu wa  MKOMBOZI  AFRICA GENERAL BUSINES
Habari za Jumapili Waungwana

MTEJA>>Habari za kazi engineer na  team nzima ya Mkombozi Africa natumia mnaendelea vizuri na kazi, Napenda kuuliza, Ivi kuna uhusiano wowote kati Earth wire na Matumiz ya umeme?
Nyumba ninayoish earth wire imeharibika haifanyi kazi yake, matumiz yang ya umeme ni ya kawaida sana, sasa tatizo ni Bill kubwa ya umeme (bill hua inacheza kat ya 15,000 to 36,000/- kwa mwez) kila nikiwauliza tanesco kwanin bill ni kubwa ivi wakat matumiz yangu ni ya kawaida siku zote? Jibu wanalonipa ni kua niangalie earth wire kam inafanya kazi, Swali langu ni Je kuna uhusiano gan kat ya earth wire na bill kubwa ya Umeme?
 
JIBU KUTOKA MKOMBOZI AFRICA
Kazi kubwa ya waya wa earth,ni kuwezesha EARTH LEAKAGE CIRCUIT BREAKER,ifanye kazi vizuri,kulinda mfumo mzima wa umeme wa nyumba inapotokea,short circuit (waya wa LIVE na NEUTRAL kugusana),au mkondo wa umeme badala ya kurudi kupitia waya wa NEUTRAL,unapitia njia nyingine,( kupita waya wa earth).

Tatizo lako linaweza kusababishwa na vitu vifuatavyo.
1.      Kama mfumo wa umeme wa nyumba(wiring)
hapa namaanisha waya zilizotumika,zitakuwa zimechoka sana(INSULATION RESISTANCE imepungua) umeme unaweza kuwa unavuja kidogo kidogo,kati ya waya ya moto LIVE(RED WIRE) na waya ya NEUTRAL(BLACK WIRE),pamoja na EARTH wire(GREEN WIRE).
Tatizo hili ufumbuzi wake ni kufanya wiring upya na kutumia waya zenye viwango bora,Test ndogo unayoweza kufanya kugundua kama unatatizo hili,ni zima kila kitu kinachotumia umeme hapo nyumbani,kama ni tv,chomoa kabisa plug,kwenye socket,au zima kabisa kwenye socket,baada ya muda wa saa 3 mpaka sita,angalia kama UNIT zako zimepungua kwenye mita


MKOMBOZI AFRICA





JE, UNAHITAJI USHAURI,UNATATIZO LOLOTE LINALOHUSU UMEME AU VIFAA VYA UMEME,JE UNAHITAJI VIFAA BORA NA IMARA VYA UMEME KWA AJIRI YA AJIRI YA NYUMBA YAKO AU OFFICE YAKO, JE, UNAHITAJI HUDUMA YA EMERGENCY NYUMBANI AU OFFICE YAKO??

Ungana na watu zaidi 500,000  waliowahi na wengine wanaendelea kufanya kazi na sisi za kununua material na  vifaa bora vya umeme, ushauri bora wa kitaalamu kutoka kwa maengineer wetu,wanafanyiwa kazi mpya, wanafanyiwa ukarabati mzuri wenye kiwango bora kwenye nyumba zao
kutoka kwetu MKOMBOZI AFRICA, kama unahitaji  huduma zetu zilizo bora  kila siku wewe wasiliana nasi kwa  
namba za simu  0716762015 au 0715751443
whatsappp namba 0716762015 au unaweza kututumia  e mail  kwenda e mail yetu inaitwa makinspire8t@gmail.com 
>>VIWANGO VYA KAZI ZETU NI BORA NA VYA UHAKIKA NA KUAMINIKA
>>   Ili kuwa karibu na habari zetu Usisahau  kulike FACEBOOK page yetu inaitwa  MKOMBOZI AFRICA ili kupata habari zote kila wakati tunapoziweka hapa au  click hapa kulike page yetu


2.      Sababu ya pili
Inawezekana mita unayotumia ina matatatizo,suala hili inabidi ulifikishe TANESCO,wao ndio pekee wenye mamlaka ya kufungua MITA zao,usijaribu kuigusa,unaweza kwenda jela mkuu.

Ushauri,unapokuwa umezima redio,au TV,muda ambao hauvitumii,sanasana wakati wa usiku,hakikisha havipo standby,yaani bado kuna vitaa vyekundu bado vinawaka,vyombo hivi vikiwa standby,umeme unatumika,zima kabisa kwenye socket ukutani,especially wakati wa usiku wa kulala,au unapokuwa umetoka,ZIMA KABISA UKUTANI,

Kwa matatizo niliyoorodhesha hapo juu,kama EARTH wire ipo,EARTH LEAKAGE CIRCUIT BREAKER,ingekuwa ina kata umeme mara kwa mara,Akikisha ELCB(EARTH LEAKAGE CIRCUIT BREAKER) imefungwa na inafanya kazi,kwa usalama wa nyumba,na vifaa vyako vya umeme.
 
Kwa kuongezea ni muhimu kutest earth leakage circuit breaker yako.
watu wengi huwa wanachanganya kutofanya kazi kwa earth wire na earth leakage circuit breaker,
ni kwamba kama EARTH LEAKAGE CIRCUIT BREAKER (ELCB) yako ni mbovu umeme unapopita njia ambayo siyo earth wire inaupeleka ardhini ili usikudhuru wewe mtumiaji,na kwa kuwa breaker yako ni mbovu haikati umeme umeme huendelea kutiririka kwenda ardhini mita hukimbia kana kwamba unatumia umeme kwa kasi,kitendo hiki kinakuingiza gharama kubwa.

Namna ya kuijaribu ELCB yako kuona kama inafanya kazi.
Ukiiangalia ELCB yako utaona kitufe kimeandikwa ''test'' ukikibonyeza kama umeme upo EARTH LEAKAGE CIRCUIT BREAKER( ELCB) yako itazima umeme mara moja,endapo haitazima,fanya utaratibu wa kukagua earth rod yako,wakati mwingine materials zinazotumika siyo KOPA  halisi na hivyo hupata kutu na kuzuia umeme kwenda ardhini kirahisi.
kama  hiyoearth  rod ni nzuri,kuna uwezekano wa earth wire yako kuwa imekatika.
ukigundua haijakatika basi zima umeme kwanza nyumba nzima kisha  angalia vizuri
shimo la earth rod ,kisha washa umeme na jaribu kubonyeza tena kitufe cha test kwenye ELCB
kama haitazima hapo fanya mpango wa kubadilisha ELCB yako.

ZINGATIA: Umeme ni hatari na unaua. kama huna uhakika na unachokifanya
Tutafute sissi ili tukufanyie kazi yako kwa ubora zaidi.

MKALA IMEANDIKWA NA ENGINEER ALEX LIMAKI TOKA MKOMBOZI AFRICA


MKOMBOZI AFRICA 


OFFICE  ZETU.


Tunapatikana  maeneo  ya  UNGINDONI-KIGAMBONI-DAR  ES  SALAAM (KARIBU NA STENDI YA DARA DARA  ZA  UNGINDONI)  AU  WASILIANA NASI  KWA ANUANI ZIFUATAZO.

SIMU>>0715-751443 (TECHNICIAN).
            0716-762015 (ELECTRICAL ENGINEER).
          E mail>>makinspire8t@gmail.com

 HUDUMA ZETU.
  •  Usambazaji wa vifaa vya umeme vya aina zote. 
  • Electrical installation (wiring za nyumba  za  aina  zote). 
  • Uchoraji ramani za wiring ya aina zote za nymba. 
  • Tunatoa  hudama  za ushauri wa kitaalamu kuhusu  umeme kiujumla. 
  • Tunafanya marekebisho/matengezo ya vifaa vya umeme  vya aina zote. 
  • Tunafanya  marekebisho  ya  wiring za zamani au zilizochoka za nyumba  za aina zote. 
  • Tunafunga  CCTV  camera. 
  • Ufungaji wa vifaa vya solar na uuzaji wa vifaa solar 
  • Tunafunga automation system za aina zote.
  •    Ili kuwa karibu na habari zetu Usisahau  kulike FACEBOOK page yetu inaitwa  MKOMBOZI AFRICA ili kupata habari zote kila wakati tunapoziweka hapa au  click hapa kulike page yetu
  • Umalizapo kusoma tafadhari sana unaombwa kushare kwa wengine ili wapate kuomba maana kazi ni muhimu.
                              MKOMBOZI AFRICA        
Suluhisho la elimu ya umeme Tembelea ➦➥ mkombozi africa
 Tahazari⇶ usifanye kazi za umeme kama huna utaaramu nayo, umeme ni hatari


0 comments: