Kama upo TANZANIA na unahitaji vifaa bora vya umeme au unashida ya kutatuliwa tatizo lolote linalohusu umeme kwenye nyumba unayojenga/uliyojenga tutafute kwa namba +255716762015(ENGINEER) AU 0715751443(TECHNICIAN) na TUTAKUJA SEHEMU ULIPO
Inaandi kwa Eng. Alex limaki
Napenda kuwakaribisha katika majadiliano ya tatizo hili
ambalo limekuwa likisababisha majanga makubwa sana hapa kwetu Tanzania kutokana
na hasa kuongezeka kwa matumizi ya umeme..
Uchambuzi nitakao utoa hapa ni kwa majibu wa elimu yangu ya
umeme pamoja ufahamu wangu juu sheria ya umeme ya kimataifa IEE regulation.
Pia uchambuzi huu utazingatia British Standard of the IET
Wiring Regulations.Kwani mfumo yetu mingi ya umemeya Kiafrika hata ule wa
Tanzania ume-copy kutoka katika regulation hizi kubwa mbili duniani.
Nasababu ya kutumia IET wiring regulation ambayo ni ya
British standard 7671 ni kwa sababu inazungumzia sheria na kanuni za umeme wa
kiwango cha 230V kwa single phase.Ambao ndiyo shirika la umeme Tanzania Tanesco
linausambaza kwenye makazi ya watu.
1.MAKOSA YANAYO SABABISHWA NA MAFUNDI WIRERING
(a). Overload of power supply wire:Hii husababishwa na line
moja ya power supply kutoka katika main switch kutumika kusambaza umeme katika
vyumba vingi.
Mfano nyumba nyingi mafundi hutumia 2.5 mm2wire kama supply
ya kwenye vyumba,supply hii hutumika kama junction supply ya vyumba vingine.
Wire ya 2.5 mm2 kitaalamu mwisho wake wa kupitisha current
kiusalama ni 20Ampere ikitokea current zaidi ya ishirini ikalazimishwa kupita
katika waya ya namna hii husababisha waya kupata moto,kama hali hii itakua
kubwa sana waya huu huungua.na huenda ukasababisha moto.
(b). Current ya Miniature Circuit Breaker(MCB) kuwa kubwa
kuliko current ya wire.
Mfano wire wa 2.5 mm2 tumeona kuwa una uwezo wa kupitisha
20Ampere kiusalama
Hivyo MCB yake inatakiwa iwe ya 20Ampere.
Lakini mafundi wengine kwa kujua au kuto kujua hujikuta
wanafunga MCB zenye current kubwa zaidi ya wire husika hali hii huweza
kusababisha wire husika kuungua kwani MCB itashindwa kujizima hata pale wire
itakapo kuwa imefikia kiwango chake cha mwisho cha kupitisha current.
Matokeo yake wire husika unaweza kuungua na kusababisha
moto.
Mfano wa MCBs;-
Viwango sahihi vya MCB na size ya waya zake zinazo shauliwa
kimataifa ni hizi hapa.
1.5 mm2 cable - 15 amp maximum circuit breaker.
2.5 mm2 cable - 20 amp maximum circuit breaker.
4 mm2 cable - 25 amp maximum circuit breaker.
6 mm2 cable - 32 amp maximum circuit breaker.
10 mm2 cable - 40 amp maximum circuit breaker.
(c). Loose Connection katika maungio ya waya na kwenye vifaa
vinavyo funga waya kwa screw.
Kama fundi hato kaza waya vizuri wakati wa kuziunga pamoja
katika viungo vya screw au waya kwa yaya ni chanzo kikubwa cha kutokea kwa
cheche ambazo hatimaye huweza kuanzisha moto.
(d). Tabia ya mafundi umeme kukubali kuunga mfumo wa
wiriring wa nyumba nyingine dhidi ya nyumba nyingine.
Kwa kawaida Tanesco huingiza umeme katika nyumba kutokana na
plan pamoja na mahitaji ya kiwango cha umeme cha nyumba husika(Kilowatt
Hour).Hili hujumuisha ukubwa wa size ya waya wa kuingiza umeme katika nyumba
yako n.k
Pia waya unao ingiza umeme kutoka katika meter kwenda ndani
ya nyumba (tell wire)mara nyingi size yake hutegemea mahitaji ya nyumba husika.
Hivyo nyumba inapo pewa umeme hua imejitosheleza kwa
mahitaji yake binafsi kitaalamu.
Inapotokea nyumba nyingine ikaungwa katika mfumo huo wakati
plan yake haikuhusishwa wakati wa kufunga umeme katika nyumba ya awali hali hii
hupelekea OVERLOAD katika tell wire hali ambayo inaweza kupelekea wire hiyo
kuungua na kusababisha moto.
2. MAKOSA YA SHIRIKA LA USAMBAZAJI UMEME
(a). Kuto funga Vilinda circuit wakati wa kufunga meter za
umeme.
Shirika la usambazaji umeme ni lazima lihakikishe linaweka
vifaa vya kulinda nyumba husika dhidi ya matatizo ya umeme.
Shirika la umeme ni lazima liweke vifaa kama vile CUT-OUT au
CRCUIT BREAKER kabla ya umeme haujaingia katika METER ya umeme au ndani ya
nyumba.
Ufungaji wa vifaa hivi ulikua unazingatiwa sana
zamani(sababu licha ya kuwa kama fuse CUT-OUT zilitumika kukata umeme katika
nyumba pale mteja akishindwa kulipa bill ya umeme).
Sasa baada ya kuingia kwa meter za LUKU imeonekana kama
CUT-OUT hazina maana tena hivyo suala lake la kutumika kama kifaa cha kulinda
mfumo wa umeme kama fuse limepuuziwa.
Kuna baadhi ya nyumba zimefungwa CUT-OUT hadi sasa licha ya
kuwa zinatumia LUKU,pia kuna wenye bahati ambao mita zao zina Circuit brekers.
Tazama picha;-
Ufungaji wa umeme usio zingatia vifaa hivi,unaongeza
uwezekano mkubwa wa kuto kea short ya umeme yenye madhara.
Kama umeingiziwa umeme katika nyumba yako halafu vifaa
nilivyo vitaja hapo juu hujafungiwa hata kimoja(yaani umeme umetoka katika
bracket na kuingia katika meter moja kwa moja bila kupitia katika CUT-OUT au
CIRCUIT BREAKER )mfumo wako wa umeme si salaama ni haki yako kufungiwa vitu
hivyo una haki ya kudai kwa usalama wa nyumba yako.
(b). Miundo mbinu mibovu ya shirika la ugavi wa umeme.
Hali hii hupelekea kutatika katika hovyo kwa umeme,hali hii
huweza kuzalisha Electrical Surges ambazo huweza kuleta madhara kwa watumiaji
wa umeme.

3. KUCHAKAA KWA WIRiRING ,VIFAA BANDIA NA VIFAA VIBOVU .
(a) Circuit breaker mbovu au feki .kuna circuit breaker
nyingine mbovu au bandia ambazo zinashindwa kujizima pale short
ikitokea,hakikisha unaijaribu circuit breaker yako mara kwa mara kwa kubonyeza
“trip test” kuona kama inafanya kazi au la.
(b) Switch za umeme na extension cables ambazo ni mbovu au
hazijakidhi vigezo(bandia)ni chanzo kikubwa cha moto katika makazi yetu.
Vifaa kama vile switch ambazo zimesha haribika vibadilishwe
ili kuepuka kutokea kwa moto.
Pia epuka kutumia Extension cables ambazo ni bandia.
(c) Wiriring iliyo chakaa huweza kusababisha kutokea kawa
moto kutokana na kulegea kwa viungo vyake ambavyo husababisha chehe,pia wire
zake huwa zimeshambuliwa sana na wanyama na wadudu hivyo zinaweza zikagusana na
kusababisha short yenye kupelekea moto kutokea.
4. KUFANYA MATENGENEZO YA VIFAA VYA UMEME NA KUVITUMIA BILA
KUWA NA UTAALAMU.
Watu wengi wamekuwa wakifanya matengenezo ya vifaa vya umeme
angali hawana utaalamu wa umeme.Vifaa vyote vya umeme ni lazima vikatengenezwa
na mtu ambaye amesomea kazi hiyo.
Mfano watu wengi hubadilisha fuse katika mifumo mbalimbali
ya vifaa vya umeme pale zinapo ungua.Ubadilishaji wa fuse hizi mara nyingi
hufanyika kiholela bila kuzingatia kiwango cha current cha fuse husika.
Hali hii husababisha fuse husika kuto kukatika wakati short
ikitokea hivyo huweza kupelekea waya kuuungua napengine kusababisha short ya
umeme.
5. KUJAZA VIFAA VINAVYO TUMIA UMEME KATIKA EXTENSION CABLE
KUZIDI UWEZO WAKE .
Extension cable zimetengenezwa kwa uwezo tofauti
tofauti.Hakikisha hauzidishi vifaa vya umeme vinavyo chukua umeme kupitia
extension cable yako ili kuepuka uwezekano wa extension cable hiyo kuungua.
SOLUTION
1. 1. Makosa haya makubwa matano yanaweza yakaepukika kwa
kila mmoja kufata utaratibu na kanuni za ndani ya nchi na za kimataifa zinazo
simamia matumizi bora ya umeme.
2. 2. Walaji wa umeme wawe na utaratibu wa kukagua mifumo
yao ya umeme mara kwa mara Kupitia wataalamu wa umeme ili kuthibitisha usalama
wa mfumo wake wa umeme katika nyumba yake.
Utaratibu huu wa ukaguzi ni muhimu ambapo mtaalamu atakagua
kama wirering system yako imekidhi vigezo;ambapo mtaalamu wa umeme hutakiwa
kuchukua vipimo maalumu na kuangalia kama mfumo wako wa umeme umekidhi kanuni
na taratibu zinazo simamia mifumo ya umeme..
Baada ya vipimo mtaalamu huyo hutakiwa kuandaa ripoti yenye
taarifa ya ukaguzi na kutoa matokeo ya ukaguzi huo wa mfumo wa umeme katika
nyumba yako.
Mkaguzi atatoa majibu makuu matatu kulingana na sheria na
kanuni za mifumo ya umeme majumbani kuwa mfumo wako wa umeme ni (Salama,Salama
kidogo unahitaji marekebisho au si salama).Report hiyo ataisaini na
kukukabidhi.
3. Ufungaji wa vifaa vinavyo tambua ishara ya kutokea kwa
moto(fire sensor)
1. 4. Kuepuka kufanya matendo ambayo yatapelekea kutokea kwa
tatizo la umeme ambalo linaweza kusababisha moto.
5.Kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika majumba yetu.
Not always electrical fault will give you a chance to
correct your mistake.BE CAREFULLY!
NA Engineer Alex Limaki
Kama upo TANZANIA na unahitaji vifaa bora vya umeme au unashida ya kutatuliwa tatizo lolote linalohusu umeme kwenye nyumba unayojenga/uliyojenga tutafute kwa namba +255716762015(ENGINEER) AU 0715751443(TECHNICIAN) na TUTAKUJA SEHEMU ULIPO