Kama
upo TANZANIA na unahitaji vifaa bora vya umeme au unashida ya kutatuliwa tatizo lolote linalohusu
umeme kwenye nyumba unayojenga/uliyojenga tutafute kwa namba +255716762015(ENGINEER) AU 0715751443(TECHNICIAN) na
TUTAKUJA SEHEMU ULIPO
Na engineer alex limaki |
Ndugu mtanzania mwenzangu
Wiki hii mwanzoni jirani yangu
aliunguliwa nyumba na alifanikiwa kuokoa vitu vichache sana. Nyumba iliteketea
kabisa kwa moto ulioanza saa tisa usiku na kudhibitiwa saa kumi na moja.
Moto huo ulianzia kwenye dari na
kusambaa paa lote kabla haujadondoka chini na kuanza kuunguza vitu vingine.
Inaonekana moto huu ulisababishwa na
hitilafu za umeme. Katika matukio mengi kama haya Tanesco huwa wanalaumiwa
lakini kwa hakika huwa hawausiki.
Kwa kawaida Tanesco anawajibika
mpaka mwisho wa meter na baada ya hapo wewe mteja ni wajibu wako kuhakikisha
usalama wa nyumba yako.
Mambo yanayoweza kuwa kisababishi
cha moto ni kama yafuatayo:
1.Kutumia nyaya ndogo zaidi ya uwezo
wa swichi.
-Mafundi wengi huwa
hawafanyi mahesabu vizuri , ununua tu nyaya na kufunga kutoka kwenye swichi
bila kuangalia uwezo wa swichi unakotoka umeme. Kazi ya swichi hizi ni kulinda
nyaya zako pamoja na vifaa vyako visiwake moto pindi umeme ukiwa mkubwa kuliko
uwezo wa waya au kifaa chako.Mfano kama switch yako ni ya amp 6 hakikisha
waya wako una uwezo wa kubeba angalau amp 8.

2. Kutumia swichi zisizozima zenyewe
kunapokuwa na tatizo
Kwa kawaida swichi (Breaker )
hupaswa kuzima mara litokeapo tatizo au umeme unaopita unapokuwa mkubwa kulipo
uwezo wake. Hii ndio njia ya kuzuia moto usitokee. Inapotokea ukafunga swichi
ambazo hazina uwezo wa kufanya hivyo unaweka nyumba na mali yako katika hatari
ya kuungua moto.
3. Kutumia swichi na nyaya
zilizotengenezwa chini ya viwango.
Kwa soko la sasa vifaa feki vimezagaa
kila mahali. Unapaswa kuwa makini unaponunua vifaa vya umeme kwa kununua katika
maduka unayoyaamini na mtengenezaji unayeamini bidhaa zake. Unaweza kununua
nyaya zilionyeshwa kuwa za ubora wa juu na kumbe ni za ubora duni. Na pia kuna
swichi nyingi zinazouzwa kwa sasa ni za viwango vya chini sana.
4, Mafundi kuweka viungio hafifu
(weak joints)
Viungio vya nyaya vinapokuwa legevu
(loose) husababisha cheche za moto ambazo ni rahisi kusababisha mlipuko kama
ziko karibu na kitu kinachoweza kulipuka, pia huanzisha moto kwa taratibu sana,
kwakuwa viungo hivi vinakuwa darini matatizo haya huwa hayaonekani mpaka tatizo
linapotokea.
Mambo ya kufanya.
1. Hakikisha mtu unayempa kazi ya
kufunga nyaya na vifaa vingine vya umeme anaelewa vyema kazi anayoifanya,
azingatie size za nyaya kulingana na matumizi na uwezo wa swichi umeme
unakotokea.
2. Swich zote kwenye swich kuu
(Main switch) Ziwe na uwezo wa kusima angalau ndani ya nusu sekunde (0.5 of
second) kunapotokea tatizo.
3. Tumia vifaa vyenye ubora .
4. Hakikisha viungio vyote vya nyaya
vimekazwa na kagua viungio hivyo angalau baada ya week moja na mara mbili
baada ya miezi mitatu mitatu.
Nakutakia jioni njema na weekend
njema.
mwandishi Engineer ALEX KIMAKI KUTOKA MKOMBOZI AFRICA
Kama upo TANZANIA na unahitaji vifaa bora vya umeme au unashida ya kutatuliwa tatizo lolote linalohusu umeme kwenye nyumba unayojenga/uliyojenga tutafute kwa namba +255716762015(ENGINEER) AU 0715751443(TECHNICIAN) na TUTAKUJA SEHEMU ULIPO
0 comments: